uwezo wa kusoma ishara za barabarani na kurekebisha mwendo wake ili kuhakikisha kuwa gari haliendi kwa kasi.
Teknolojia
hiyo inatumika kwa kutumia usukani wa gari na inaweza kutolewa kwa
kutumia kikanyagio cha kuendesha gari iwapo dereva atakanyaga kikanyagio
hicho cha mafuta kwa nguvu.
Kampuni hiyo ya magari inapendekeza
kwamba kifaa hicho kitawasaidia madereva kukwepa kulipishwa faini na pia
huenda kikapunguza idadi ya ajali.
Hatahivyo mtaalam mmoja amesema kuwa teknolojia hiyo itatumika kwa mda mfupi.
''Kuna
mpango wa kudhibiti kasi ya gari lako kupitia kifaa kitakachowekwa
katika kompyuta ya gari hilo na kudhibitiwa kutoka eneo hilo,badala ya
kutafuta kifaa cha kusoma ishara za barabarani'',alisema Paul Newton
mshauri wa maswala ya magari.
''Hii ni miongoni mwa mikakati
itakayounganisha mifumo ya magari ,na kuyafanya magari kuonya magari
mengine yalio nyuma yao iwapo yanataka kupunguza mwendo ikiwa ni kati ya
mipango ya kutengeza magari yanayoweza kujiendesha.