Mitandao ya Intaneti inatumika na watu wa aina mbali mbali duniani kwa madhumuni tofauti tofauti. Kwa ufupi hapa leo tutaangalia matumizi yako ya Intaneti na kutathmini kwa ufupi sana matokeo ya matumizi yako ya Intaneti kwa maisha yako na hatimae unaweza ukajiuliza mwenyewe maswali ya msingi kama:
- Unatumiaje Mitandao
- Huwa unaangalia tu taarifa mitandaoni?
- Je kuna lolote unajifunza mitandaoni, unafurahishwa navyo, au yanakusaidia katika kuendesha maisha yako?
- Na je unadhani matumizi yako ya mitandao ni ya aina gani? Je yanawiana na umri, aina ya maisha unayoishi, kundi, utaifa au taaluma yako?
Nisikuchoshe. Kwa ufupi fanya yafuatayo ukiwa bado katika browser yako :
- Bonyeza kitufe cha Ctrl na wakati huo huo bonyeza herufi H kwenye keyboard yako.
- Click kwenye kichwa cha "Today" kwenye historia ya browser yako
- Bonyeza Ctrl na A kwa wakati mmoja ili ukopi
- Kisha Paste ulichokopi kwenye historia ya browser yako kwenye kijedwali jekundu la kulia hapa
- Bonyeza kitufe cha "Visualise" kutathmini historia ya browser yako
Baada ya hapo utajionea majedwali mbali mbali yanayokuonyesha ni aina gani ya tovuti ambazo huwa unazitembelea mara kwa mara. Itakuonyesha Ni aina gani ya huduma tovuti hizo hutoa. lakini pia itakuonyesha ni maeneo gani ya maisha mitaondao inahusika au huhusiki navyo nawe na nini unapendelea maishani mwako