MWANZILISHI
mwenza wa kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya mawasiliano ya Obi
Mobiles, yenye makao makuu yake Singapore, John Sculley amesema ujio wa
kampuni hiyo nchini Tanzania, utaongeza wigo wa utumiaji wa tehama na
hasa matumizi ya zana za kisasa za mawasiliano.
Obi Mobile inatumia teknolojia iliyobuniwa mjini Toronto, Canada na kampuni ya Inflexionpoint.
John
Sculley, ambaye alishawahi kuwa ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Apple
amesema teknolojia hiyo mpya ambayo ilizinduliwa India na Mashariki ya
Kati mwaka 2014 imelenga kuwanufaisha vijana ambao ndio watumiaji wa
kubwa wa simu za kisasa.
Amesema
kwa kuingiza bidhaa za Obi nchini Tanzania wanatarajia kuwawezesha
vijana kuwa na simu ambazo zinawatumikia wao kwa maarifa na umaridadi
zaidi.
S550-Hornbill.
“Simu hizi zimepokewa vyema zilikozinduliwa na tunararajia Tanzania nazo watazipokea kwa kasi hiyo hiyo” alisema Sculley .
Kwa mujibu wa ofisa huyo, simu za Mobile nchini Tanzania zinauzwa kati ya sh 50,000 na bei ya juu ni 350,000.
Alizitaja
aina hizo za simu kuwa ni Hornbill S551; Falcon S451; Crane S550;
Wolverine S501; Fox S453 ; Racoon S401 na Power GO F240 simu ambayo
ina betri yenye uwezo wa 2,800mAH na yenye uwezo wa kuchaji simu
nyingine.
Amesema
watu wa Obi Mobiles wanaamini kwamba teknolojia ni kwa ajili ya watu
wote na ndio maana mauzo ya teknolojia zao ni rahisi kwa ajili ya watu
wote.
Alisema kwa kuwa na vifaa vya teknolojia ya Obi, vijana watakuwa na nafasi ya kutumia fursa zilizopo za kiuchumi na kijamii.
S453-Fox
Sculley
amesema kwa muono wake teknolojia haitakiwi kuwa ngumu kuitumia wala
kutengeneza changamoto kwa watumiaji wake kwa kuiwekea vikwazo.
Teknolojia
za Obi Mobile zinazotumia mfumo wa Android ni za daraja la juu na
wkamba simu zote za Obi zilizoingizwa nchini zina uwezo wa kuwa na
intaneti.
Kampuni hiyo inatarajia kuzindua simu hizo nchini Tanzania mwezi ujao .
Akizungumzia
mkakati wa kampuni hiyo kwa bara la Afrika , Mkurugenzi Mtendaji wa Obi
Mobile MENA, Amit Rupchandani: “Walaji wengi wanataka kujiondoa katika
simu za kawaida kwenda katika simu za kisasa. Hata hivyo,gharama za
uwekezaji katika teknolojia ya kisasa ni kikwazo kikubwa kwa watu
wengi.”
Obi
Mobiles, wamesema kwamba kwa kuelewa hilo, wamewezesha kuwa na simu
zenye uwezo mkubwa na kwa bei nafuu ili kufikia kila kundi katika bara
la Afrika.
Simu hizi ambazo vijana watazipenda zimeelezwa kutengenezwa kumudu maisha yao na kuwapendezesha